Mmoja ya washiriki wa Mafunzo ya Epicor 10.2 akitoa msaada wa kiufundi wakati wa mafunzo hayo
Bibi Shani Mangesho Ofisa Msimamizi wa fedha mwandamizi katika Mkoa wa Tabora akiwa katika mtihani wa kuwapima Wekahazina na Wahasibu wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2 jijini Mwanza
Washiki wa Mafunzo, wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mfaume Mnokote hayupo pichani wakati wa somo la Msaada wa dharura wakati wa mafunzo ya Epicor 10.2 mkoani Mwanza (Picha zote na Atley Kuni wa OR TAMISEMI)
Atley Kuni na Glady
Mkuchu- Mwanza
Washiriki wa Mafunzo
ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka mikoa nje (Non PS3 Region) ya mradi wa
uimarishaji mifumo ya sekta ya umma PS3 katika mkoa wa Mwanza, wameiomba
Serikali ione namna itakavyoweza kukaa na wadau hao ili mradi uweze kuhudumia
nchi nzima badala ya sasa ambapo upo katika Mikoa 13 na Halamshauri 93 pekee.
Ombi hilo limetolewa na Wekahazina pamoja Wahasibu kutoka Halmashauri
za mikoa ya Tabora na Geita ambao wamekuwepo katika mafunzo ya siku nne ya Mfumo
wa Usimamizi wa Fedha za Umma (Epicor) Toleo 10.2, ambapo mara baada ya mafunzo
hayo watendaji hao wataanza kuutumia mfumo huo ifikapo Julai mosi, 2018.
Nicholaus John ni Mwekahazina
katika Halmashauri ya Wilaya Chato mkoani Geita, yeye anasema pamoja na uzuri
wa mifumo lakini wanapendekeza kuwa mradi pia uweze kufikiria kutekeleza na
kufika katika mikoa mingine ili kuweza kuleta uwiano sawia katika utekelezaji
wa mifumo ya Umma .
Nicholaus anaongeza
kuwa , matunda ya ukusanyaji mzuri wa mapato katika Halmashauri zao umetokana
na kuwa na mifumo imara ambayo inasimamiwa na TAMISEMI lakini pia ufadhili kutoka
kwa Shirika la Misaada la Marekani
(USAID) kupitia mardi wa PS3.
Akitoa maoni yake
Shani Mangesho, Afisa Msimamizi wa fedha katika Mkoa wa Tabora anakiri kuwa PS3
imefanya kazi kubwa kwenye mifumo lakini bado wanayohamu yakuona mradi huo
unaongeza eneo la ufadhili.
Mbali yakuomba mradi
huo uweze kwenda nchi nzima, lakini Wekahazina hao na Wahasibu hawakusita
kuelezea furaha yao ya mabadiliko ya mara kwa mara yanayoendelea kufanywa na
Serikali hasa katika kuimarisha mifumo ya Sekta ya umma.
Zablon Nashokigwa
Mwekahazina Halmashauri ya Wilaya ya urambo,
alisema mafunzo ya Epicor 10.2 kwa wataalam wa kada za wahasibu yamekuja kwa
wakati muafaka kwakuwa mifumo mingi sasa itafungamanishwa na mfumo huo.
“Nawashukuru TAMISEMI
na PS3 katika kutujengea uwezo, hii kwetu itakuwa chachu ya uboreshaji wa
shughuli zetu za kila siku hasa katika eneo la upatikanaji wa taarifa kwa muda muafaka.Kutokana
na mfumo huu kuwa Kimtandao (Web based) ambao utamwezesha mtendaji kufanya kazi
mahali popote ambapo yupo tofauti na mfumo ambao tunakwenda kuachana nao
ifikiapo Julai Mosi,” amesema Nashokigwa.
Marietha Masanja
kutoka Halmashauri ya Geita Mji amesema“Katika Epicor.10.2 hakutakuwa na hundi
isipokuwa malipo yote yatafanyika kwa mfumo wa (Tanzania Interbank Settlement
System-TISS) ambayo imeunganishwa kwenye mfumo huu ulioboreshwa, hivyo
itawaepusha wahasibu na jukumu la kubeba pesa taslimu” alisema Marietha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.