ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 13, 2018

JEH KWA MPANGO HUU WA TIMUA TIMUA IKO WAPI NAFASI YA HISPANIA KUTWAA NDOO YA DUNIA?

Mkurugenzi wa michezo wa nchini Hispania, Fernando Hierro ametangazwa kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Ulen Lopetegui aliyetimuliwa hii leo siku ya Jumatano ikiwa ni mara baada tu ya kuchaguliwa na kuridhia kuwa kocha ajaye wa klabu bingwa UEFA Real Madrid.
Huyu ndiye Ulen Lopetegui, kocha aliyetimuliwan kuifundisha Hispania..


Hierro atakuwa kwenye majukumu mazito siku ya Ijumaa pale timu yake ya Hispania itakapo wakabili Ureno kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa kundi B.

Nahodha huyo wazamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid ataiwakilisha nchi yake kwa mara ya kwanza kwenye benchi la ufundi akiwa kama kocha kwenye dimba la Krasnodar.

SWALI:-
Kocha mpya kwa Hispania nyakati hizi za mwisho saa chache kabla ya filimbi ya kwanza kuashiria kuanza kwa Kombe la Dunia 2018 Jeh kwako shabiki unapunguza maksi za timu hiyo kutwaa ndoo ya Dunia?
#SportsRipoti 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.