Afisa mmoja wa jeshi la Somalia ametangaza habari ya kujeruhiwa watu saba katika shambulio la kujiripua kwa mabomu lililofanywa na gaidi mmoja wa al Shabab katika kambi moja ya kijeshi iliyoko kusini mwa nchi hiyo, usiku wa kuamkia leo.
Mripuko wa bomu nchini Somalia
Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kumnukuu afisa huyo anayejulikana kwa jina la Hussein Ali akisema kuwa wanajeshi saba wa Somalia wamejeruhiwa baada ya gaidi mmoja wa al Shabab kujiripua katika gari alilokuwa analiendesha karibu na kambi hiyo katika viunga vya mji wa Kismayo, kusini mwa Somalia.
Afisa huyo wa jeshi la Somalia ameongeza kuwa, wanajeshi wa Somalia walilishambulia kwa risasi gari hilo kabla ya kuingia ndani na kumlazimisha gaidi huyo kujiripua nje ya kambi hiyo.
Ijumaa usiku pia kambi hiyo ya kijeshi ilishambuliwa na magaidi wa al Shabab na kuua wanajeshi 12 na kujeruhi wengine wanne.
Hadi mwaka 2011, magaidi wa al Shabab walikuwa wanadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Somalia kabla ya kufurushwa katika miji mkubwa na kubakia kwenye vijiji vya mbali vya nchi hiyo.
Jeshi la Somalia limeshindwa kuwaangamiza kikamilifu magaidi hao na hivi sasa wameongeza mashambulizi yao yanayoathiri pia nchi jirani kama vile Kenya.
Jeshi la Somalia lina upungufu wa vifaa na uongozi mbovu na hivyo inakuwa vigumu kukabiliana na vitisho vya genge la kigaidi la al Shabab.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.