Meneja Miradi wa Foundation for Civil Society Bw Francis Uhadi akiongea na wana azaki katika mafunzo ya siku tatu ya kuzijengea uwezo asasi za kiraia zinazofadhiliwa na shirika hilo mapema jana jijini Dododma.
Taasisi ya uwezeshaji wa asasi za kiraia ya Foundation for Civil Society (FCS) inaendesha mafunzo ya siku tatu kwa asasi zote inazozifadhili kwa sasa. Mkutano huu wa mafunzo unashirikisha asasi za kiraia (AZAKI) zinazotekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
Maeneo haya ni pamoja na uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu, vijana, wanawake, haki za raia na demokrasia pamoja na ushiriki wa wananchi katika michakato ya maamuzi, mipango, bajeti, utekelezaji na ufuatiliaji katika sekta za huduma za umma na watendaji wake
Akiongea mapema jana tarehe 25 juni 2018 kuhusu mkutano huo wa mafunzo, Meneja Miradi wa Foundation for Civil Society Bw
Francis Uhadi, amesema mafunzo haya yatachukua siku tatu yakishirikisha asasi
119 kutoka mikoa 22 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
“Kuna mambo mengi ya kuongea
kwenye agenda, yote yanalenga upitiaji wa mipangokazi na bajeti za miradi yote
inayofadhiliwa na Foundation kwa sasa. Na hatua hii huwa tunaifikia baada ya
kupitia asasi zote kila mwaka ili kutambua mapungufu ya kiufundi na changamoto
nyingine katika utekeleaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya asasi hizi”
ameongeza Bw Uhadi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini semina hiyo.
Imetolewa
na Mkurugenzi Mkuu, Foundation for Civil Society
Kwa kifupi kuhusu
Foundation for Civil Society
FCS ni taasisi iliyo huru isiyo ya kiserikali na wala
isiyojiendesha kibiashara iliyojikita kwenye utoaji wa ruzuku na kujenga uwezo
kwa asasi za kiraia nchini (AZAKI). Ni kati ya tasisi kubwa za aina hii nchini,
Afrika ya Mashariki na Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara. Imekua ikifanya kazi
ya kujenga AZAKI kwa miaka 15 mpaka sasa.
Taarifa zaidi,
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia: information@thefoundation-tz.org au kupitia namba 0767654252.Unaweza
pia kufollow hapa kwa taarifa zaidi - Twitter: @FCSTZ na Facebook: FCSTZ
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.