Hiyo itakuwa fainali ya 63 ya michuano hiyo inayoandaliwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), na msimu wa 26 tangu ipewe jina jipya la Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka lile la zamani la Klabu Bingwa Ulaya.
Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa fainali ya UEFA Europa 2018 katika Super Cup ya UEFA. Pia watafuzu kuanzia hatua ya Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mwaka 2018 FIFA kama wawakilishi wa UEFA Mabingwa watetezi, Real Madrid walitinga fainali ya 16 ya rekodi baada ya ushindi wa 4–3 jumla dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani wakiwatupa mashindanoni kwa mara ya pili mfululizo.
Na hii ni fainali ya tatu mfululizo ya Real Madrid na fainali ya nne kwenye mashindano matano huku ikipewa nafasi ya kushinda taji la 13 la rekodi, baada ya awali kushinda katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 na 2017; na kufungwa katika fainali za 1962, 1964 na 1981.
Liverpool wameingia fainali ya nane, na ya kwanza tangu mwaka 2007, ambayo walishinda kwa jumla ya mabao 7–6 dhidi ya Roma ya Italia.
Wameshinda taji hilo mara tano katika miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005, na wamefungwa mara mbili kwenye fainali 1985 na 2007.
Mwandishi mmoja aliyehudhuria mazoezi ya Real Madrid jana aligongwa usoni na mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo na kuchanika kidogo jirani ya jicho.
Real walikuwa wanafanya mazoezi Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev kuelekea fainali leo na ndipo Ronaldo alipompiga na mpira mwandishi huyo. Lakini Ronaldo alimuomba msamaha kwa ishara ya mkono mwandisi huyo aliyepatiwa huduma ya kwanza uwanjani hapo.
Beki ghali aliyesajiliwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 75 amesema kwamba Real Madrid hawajawahi kukutana na timu kama yao kabla.
Amesema; nani anajali? Alipoulizwa kama Wekundu hao walistahiloi kufika gainali ya Ligi ya Mabinghwa Ulaya.
Mashabiki wa Liverpool walishambuliwa na wababe mjini Kiev juzi, kabla ya Polisi kuthibitisha watu wawili walikamatwa.
Picha za kutisha zimeonyesha watu wakishambuliana kwa kwa magongo, meza na viti. Polisi wa Merseyside wamesema wana taarifa za tukio hilo na wana Maofisa wao mjini Kiev.
Gwiji wa England, David Beckham amemtaka mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane sasa kocha wa klanbu hiyo kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool: 'Tafadhali wafunge Liverpool'
Beckham ni mpenzi wa Manchester United ambao ni wapinzani wa Liverpool.
Beckham aliondoka Old Trafford kuhamia Los Blancos kwa dau la Pauni Milioni 25 mwaka 2003.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.