ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 7, 2018

UKO WAPI MSTARI UNAOTENGANISHA HABARI ZA UCHUNGUZI NA HABARI ZA UCHOCHEZI?


KATIKA zama hizi tasnia ya habari nchini imeshuhudia wimbi la baadhi ya wadau, si wanasiasa pekee bali hata wafanyabiashara ima watu wenye majina, nyadhifa au hata hadhi kubwa ndani ya jamii, kuwa na mtazamo hasi pale wanapokosolewa, mtazamo ambao upo mpaka kwa baadhi ya watendaji Serikalini.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Osoro Nyawangah sanjari na wadau wengine wa sekta hiyo, ndani ya kusanyiko la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kimkoa katika ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza, hapa ana weka mezani hoja yake yenye swali la kutaka kujua "Jeh mstari unaotenganisha Habari za Uchunguzi na Habari za Uchochezi unasimamia wapi?" 

Mgeni Rasmi kwa Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.