NA ZEPHANIA MANDIA, GSENGO TV
Ni maonesho kwa njia ya ushindani ambayo yamefanyika katika himaya ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha Cha IFM tawi la Mwanza, yanayotumika kama sehemu ya kupima uelewa wa wanafunzi wanaotaraji kuhitimu zama za usoni ambapo hapa wanazama katika utendaji kama wako kazini wakifafanua kwa vitendo masuala wanayohusika nayo.
Kwa mujibu wa mmoja wa Waadhiri wa chuo hicho Dr Lawrence Joseph anasema kuwa Maonesho hayo pia yametumika kama sehemu ya kuwasukuma vijana kwenye ukomavu wa kujieleza hasa pale wanapoitwa kwenye usaili wa ajira mbalimbali nchini na tukio hilo sasa linatumika kama mbinu ya kupanua wigo wa wakufunzi kuzinasa ajira.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.