Maofisa waandamizi wa ABinBev wakifuatilia matukio na shamrashamra wakati wa hafla ya uzinduzi
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa TBL wakiburudika wakati wa uzinduzi huo
Shamrashamra mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi
Shamrashamra mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi
Wageni mbalimbali wakifuatilia matukio na kupata burudani wakati wa uzinduzi. *Kuwazawadi wateja wake kushuhudia mechi za mashindano hayo Live
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited mwishoni mwa wiki imetangaza ushirikiano wake na shirika la Soka Duniani (FIFA), ambapo bia yake ya Kilimanjaro, imetangazwa kuwa bia rasmi ya Tanzania katika mashindano ya Kombe la Dunia 2018 yatakayofanyika nchini Urusi.
Kutangazwa huku kunaenda sambamba na kuzinduliwa kwa promosheni kubwa ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania itakayowazawadia wateja wa bia ya Kilimanjaro nafasi ya kujindia safari ya kushuhudia baadhi mechi za kombe la dunia nchini Urusi mubashara na pia kujishindia muda wa maongezi 2,500/= kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma number iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki Kumi.
Hafla kubwa ya uzinduzi iliyojumuisha wafanyakazi wa TBL,Waandishi wa habari,wasanii na wadau mbalimali wa kampuni ilifanyika katika kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi utaendelea kufanyika katika mikoa mingine
Meneja Masoko, udhamini na program za wateja Afrika Masharariki wa kampuni ya TBL Group Bwana George Kavishe alisema “Tunayo furaha chapa yetu maarufu ya Kilimanjaro kutangazwa kuwa bia rasmi ya Tanzania katika msimu huu wa kombe la Dunia la FIFA 2018, kampuni inatangaza kuzindua kampeni maalumu ambayo itawawezesha wateja watakaobahatika kushinda kugharamiwa safari ya kwenda Urusi kuangalia mechi za kombe la Dunia mubashara sambamba na zawadi za fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni moja kila wiki, muda wa maongezi 2,500 kila unaposhiriki kutuma number iliyopo chini ya kizibo mara 6, pamoja na zawadi kem kem zitakazotolewa kwenye promosheni za kwenye mabaa zaidi ya mia tatu nchi nzima.
Alisema washindi wapatao 10 watawezeshwa kugharamiwa kuona mashindano ya kombe la Dunia na washindi wengi wataweza kujishindia fedha taslimu, na muda wa maongezi. “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”.Alisisitiza
Ili kujishindia zawadi mteja anapaswa kutuma namba zilizopo kwenye chupa za bia ya Kilimanjaro kwenda namba 15451 ili kujipatia fedha taslimu na muda wa maongezi, Zawadi ya ticket ni kwa wale wataoshiriki kujibu maswali yatakayoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.Kililager.com na kujipatia point za ushindi.
Promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na litaendeshwa nchi nzima na matangazo yake yamezinduliwa rasmi pia kupitia televisheni, radio na mitandao ya kijamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.