NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV.
Waziri wa tamisemi SULEIMAN JAFFO amempongeza
mkurugenzi mtendaji, KIOMONI KIBAMBA, wa halmashauri ya jiji la Mwanza kwa kuridhishwa
na miradi ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Jaffo ametembelea miradi hiyo ikiwemo ukarabati
wa shule kongwe ya wasichana Nganza sekondari.
Ziara ya waziri Jaffo jijini Mwanza inaanza kwa
kukagua miradi mbalimbali iliyotekeleza katika halmasahuri hiyo, kubwa kati ya
miradi hiyo ni utayari wa jiji hili kuona kuana haja ya kupunguza msongamano
katika jiji hili kwa kutenga eneo la maegesho ya magari ya mizigo.
Hekari 23 zimetengwa katika eneo la buhongwa nje
kidogo ya jiji la Mwanza lengo ikiwa ni kupunguza msongamano pamoja na kuengeza
mapato kwa jiji hilo.
Akiwa katika eneo hilo JAFFO ameeleza
kufurahishwa na hatua ya jiji la Mwanza kubuni mradi huo ambao utaongeza mapato
kwa halmashauri na kupunguza msongamano katikati ya jiji.
Awali alianza kwa kukagua maboaresho ya shule ya
wasichana ngaza ambapo zaidi ya shilingi milioni 900 zimatumika kuboresha shule
hiyo ambayo kwasasa inakabiliwa na changamoto ya gari la kuhudumia wanafunzi.
Halmashauri ya jiji la mwanza limefanikiwa
kuanzisha na kuboresha miradi mbalimbali ikiwemo ya afya,miundo mbinu ,elimu
pamoja na machinjio ya kisasa ,huku ikiwa na malengo ya kuboresha stendi kuu ya
mabasi nyegezi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.