ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 16, 2018

CHUI ALIYEKULA MTOTO ASAKWA.

Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa nchini Kenya imeanza msako wa chui aliyekula mtoto mwenye umri wa miaka mitatu karibu na hifadhi maarufu ya ‘Queen Elizabeth’, Ijumaa usiku.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo wa kiume aliishimia mikononi mwa chui baada ya kujaribu kumfuatilia mlezi wake aliyetoka nje ya hotel ambayo haijazingirwa. Kwa mujibu wa msemaji wa hifadhi hiyo, Bashir Hangi, Mlezi wake huyo ni mfanyakazi katika hifadhi hiyo.

Mlezi huyo hakufahamu kama mtoto alikuwa anamfuata. Alisikia kelele za mtoto akilia kuomba msaada, alijaribu kuingilia lakini alichelewa, chui alikuwa ameshamkamata mtoto na kutokomea naye porini. Msako ulianza haraka na mwisho tulipata fuvu la mtoto huyo siku iliyofuata,” alisema Hangi.

Alisema kuwa wanaendelea kumtafuta chui huyo na kumuondoa kwenye hifadhi kwani mnyama anapokula binadamu anaweza kutamani kula binadamu mwingine hali inayoleta hatari Zaidi.

Mtaalam wa wanyama pori anasema kuwa ni nadra sana kwa chui kumuwinda binadamu, na kwamba hufanya hivyo pale tu anapokutana naye na hana namna.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.