GSENGOtV
CHE LSEA jana ilitwaa ubingwa wa Kombe la FA, baada ya kuwachapa Manchester United bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Dimba la Wembley jijini London.
Huu ulikuwa mchezo wa mwisho kwa timu za Ligi Kuu England msimu huu na ubingwa huu unaweza kumfanya kocha Antonio Conte aongezewe mkataba mwingine kwenye timu hiyo na kupunguza presha ya kutimuliwa.
Staa wa Chelsea, Eden Hazard ndiye alikuwa shujaa kwenye mchezo huo baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 22 ya mchezo huo, baada ya kuchezewa madhambi na beki Phil Jones.
Hata hivyo, baada ya bao hilo Manchester United walicharuka, lakini mashambulizi yao mengi yalishindwa kuwapa bao na kujikuta wakimaliza mchezo huo bila bao.
Hata hivyo, dakika kumi za kipindi cha kwanza Chelsea walionekana kuwa bora sana huku wakikosa nafasi kadhaa za wazi.
Safu ya ushambuliaji ya Manchester United haikuwa na makali yaliyozoeleka baada ya kumkosa mshambuliaji wake, Romelu Lukaku ambaye alianzia kwenye benchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.