ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 25, 2018

UZINDUZI WA ZOEZI LA KUGAWA VITABU JIJINI MWANZA.

 Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongela amezindua zoezi la ugawaji wa vitabu kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu katika shule za msingi za halmashauri ya Jiji la Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amekabidhi vitabu vya Masomo ya kuandika,kusoma,Afya na mazingira,Michezo na sanaa,maarifa ya jamii na kiingereza vilivyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI vyenye thamani ya bilioni 1.3 kwa ajili ya darasa la 1,2, na la tatu kwa ajili ya Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni idadi ya vitabu 500,446.


Lengo la Serikali ni kuhakikisha uwiano unakuwa kitabu 1kwa Mtoto 1. Mhe Mongella: Makabidhiano hayo yamefanyika s/m Buhongwa.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.