ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 25, 2018

BWENI LA WASICHANA SENGEREMA ISLAMIC LATEKETEA KWA MOTO



NA.ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV.
Bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Sengerema Islamic mkoani Mwanza limeteketea kwa moto na kusababisha wanafunzi 30 kukosa mahali pa kulala huku vifaa vyao ya shule vikitetea kwa moto vikiwemo madaftari ,vitabu,magodoro pamoja na nguo zao. 

Ni Shule ya Sekondari ya Sengerema Islamic iliyopo Wilayani Sngerema Mkoani Mwanza ambayo bweni la wasichana limeteketea kwa moto huku chanzo cha moto huo kikidaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyotekea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani wanajisomea.

Kutokana na  wilaya ya Sengerema kutokua na gari la zima moto ,inaelezwa kuwa pindi ipatapo majanga ya moto  hutegemea huduma za zimamoto zilizopo mkoani Geita ambapo kuna umbali wa zaidi ya kilometa 60 kufika wilayani humo.

Hawa ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Sengerema Islamic ambako ndiko  bweni la wasichana limeteketea kwa moto hapa wanaeleza hasara zilizopatikana kutokana na moto huo.

Yusuph Shabani ni mkuu wa shule ya Sekondari ya  Sengerema Islamic  na Hamis Mwagao maarufu kama (Tabasamu)ndiye mkurugenzi wa shule hiyo hapa wanaelea hali ilivyo na kuiomba serikali kuwapelekea huduma ya zimamoto wilayani humo.  
Emmanuel Kipole,ni mkuu wa Wilaya ya Sengerema hapa anaeleza mipango ya serikali katika kuhakikisha kuwa wanakua na gari la zimamoto wilayani humo.

Ajali hiyo ya moto iliotokea katika shule ya sekondari ya Sengerema Islamic na kuteketeza bweni la wasichana  imesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 38.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.