ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 19, 2018

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAFANYABIASHARA IKULU KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZAO.Rais Magufuli Akutana na Wafanyabiashara Ikulu Kusikiliza Changamoto Zao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt John Magufuli, Leo Machi 19, 2018, ameongoza Mkutano wa 11 wa baraza hilo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Dhumuni la Mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya biashara nchini, na namna ya kutatua changamoto zinazoikwamisha sekta hiyo kuendelea kuku na kupanuka kimataifa zaidi. Kauli mbiu ya baraza hilo ni “Tanzania ya viwanda - ushiriki wa sekta binafsi”. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Elisante Olegabriel, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majliwa, Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri mkuu, Sera, Bunge, Watu Wenye Ulemavu na Vijana, Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Nk. Aidha mkutano huo umehudhuriwa na Wafanyabiashara Mashuhuri nchini akiwemo, Mohamed Dewji 'MO', Mkurugenzi wa IPP Reginald Mengi, Said Salim Bakhresa na wengine wengi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.