ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 18, 2018

NI MOHAMED SALAH TENA NA SAFARI HII APIGA 'SUPER HAT TRICK'.


Mohamed Salah katupia mpira kambani mara nne na kuipa mabawa Liverpool kuchumpa hadi nafasi ya tatu kunako msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuinyuka Watford kunako dimba la Anfield.
Akicheza kwa kasi na umahiri Salah mapema katika mchezo huo alifanikiwa kuwahadaa walinzi wa Watford's na kuipatia timu yake goli la kwanza kabla ya kufanya hivyo tena wakati timu hizo zikielekea mapumziko mara baada ya kupokea tena pande la krosi kutoka kwa Andy Robertson's.
Alitengeneza nafasi ya goli la tatu safari hii likitoka toka kwa mchezaji mwenye akili ya ufungaji magoli ya ajabu na ufundi Roberto Firmino's , kisha akaongeza mengine mawili kukomelea msumari wa mwisho kwenye jeneza Watford.
Liverpool sasa wameongeza deni la pointi saba kwa Chelsea walio kwenye nafasi ya tano.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.