NAIBU kamishna wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Ahmed Msangi, amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu watakaobainika kutumia vibaya mitandao ya kijamii katika kuvunja sheria za nchi, kupotosha jamii au kuhamasisha vitendo vya uhalifu.
Aidha Msangi amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tayari limejidhatiti na muda wote liko fiti kwani kama askari anavyotakiwa kuwa tayari muda wote.
Kuhusu suala la maandamano Kamanda Msangi amesema sula hilo halina mjadala na kilichobaki ni utekelezaji tu.
"MAADAMANO YAMEPIGWA MARUFUKU KOTE NCHINI AMBAPO HATA AMIRI JESHI MKUU WA NCHI RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, AMELISISITIZA HILO ILI TAIFA LIFANYE KAZI, SASA YULE ANAYEKAIDI HAJITAKII MEMA" Amesisitiza Msangi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.