Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye katika picha ya pamoja na Kikosi cha Maokozi cha Jeshi hilo, wakati alipotembelea Kikosi hicho kilipokuwa kikionesha zoezi la maokozi, kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Bashiri Madhehebi ambaye ni Mkuu wa kikosi hicho.
Wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo pichani), jinsi wanavyoweza kufanya maokozi katika maji alipotembelea eneo la daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni walipokuwa wakifanya zoezi hilo, mapema leo asubuhi (kushoto) ni Sajini wa Zimamoto Salehe Salla na aliyevaa boya maalum kwa ajili ya maokozi ni Koplo wa Zimamoto Omary Katonga.
Mzamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini wa Zimamoto Saidi Sekibojo akiwa katika mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.
Sehemu ya Askari wazamiaji
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Koplo Omary Katonga (kulia)
wakionesha utimamu mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo picha) mara
baada ya kufanikiwa kumuokoa mhanga aliyekuwa kazama katika kina kirefu cha
maji, wakati wa mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere
mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi
ajali zinapotokea.
(Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.