Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema mchezo wa kesho ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake na PSG ya Ufaransa sio ushindani wa mchezaji mmoja mmoja bali ni mchezo wa timu mbili.
''Watu wanaongelea zaidi Cristiano Ronalo na Neymar kama wanacheza wawili kitu ambacho si kweli, huu ni mchezo wa Real Madrid dhidi ya PSG kwahiyo timu nzima inatakiwa kucheza'', amesema.
Aidha Zidane ameongeza kuwa hawezi kuzuia watu kuongelea nyota hao wawili kwani wanakutana mchezaji ghari zaidi ulimwenguni na mchezaji bora duniani kwahiyo kunakuwa na sababu ya ziada ya watu kuongea lakini hawachezi peke yao.
Zidane pia amesema wao kama Madrid licha ya kutokuwa na msimu mzuri lakini hawana presha na mchezo huo na wanafurahia kucheza aina hiyo ya mechi.
Real Madrid inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga ikiwa nyuma kwa alama 17 dhidi ya vinara Barcelona wenye alama 59.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.