ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 26, 2018

VIDEO WATUHUMIWA KESI YA KUTAFUNA MALI ZA CHAMA CHA USHIRIKA NYANZA WARUDISHWA RUMANDE.


PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO TV
Jaji  wa mahakama kuu  kitengo cha Uhujumu Uchumi, Firmin Matogoro ameitupilia mbali hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya DPP iliyowasilishwa kupinga dhamana  dhidi ya Watuhumiwa wawili wa kesi ya uhujumu uchumi  Timoth Kilumile na Anthonia Zakaria wanaokabiliwa na Mashtaka ya  ubadhirifu wa mali za chama kikuu cha ushirika cha Nyanza  zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bil.10.

Hati hiyo ya Mkurugenzi wa mashtaka iliyotaka mahakama kuzuia dhamana ya watuhumiwa katika kesi kwa madai ya kutaathiri usalama na  maslahi ya jamuhuri jaji Frimani amesema hoja hiyo haina mashiko kwakua watuhumiwa walitenda kosa hilo mwaka miaka 16 iliyopita  na hakuna athari zilizotokea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.