TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 13.02.2018
¨ WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 104.4, WILAYANI
ILEMELA.
KWAMBA
TAREHE 12.02.2018 MAJIRA YA SAA 20:58HRS USIKU KATIKA MTAA WA KILOLELI KATA
NYASAKA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
SHAFII ABDALLAH, MIAKA 21, MKAZI WA MTAA WA NYAMANORO NA 2. JOHN JOHN, MIAKA
19, MKAZI WA MTAA WA KITANGIRI, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA
KUPATIKANA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 104.4, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI
POLISI WAKIWA DORIA WALIPOKEA TAARIFA
TOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU WAPO WATU WANAOJIHUSISHA
NA UUZAJI NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI. AIDHA BAADA YA
POLISI KUPOKEA TAARIFA HIZO WALIFANYA
UPELELEZI NA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO NA BAADAE WALIFANIKIWA KUMKAMATA
MTUHUMIWA WA KWANZA AITWAYE SHAFII ABDALAH AKIWA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 38
NA BAADAEA ALIKAMATWA MTUHUMIWA MWINGINE AITWAYE JOHN JOHN AKIWA NA BHANGI
KIASI CHA GRAMU 66.4.
POLISI
WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE
WANAOSHIRIKIANA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU KATIKA
BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI BADO UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA
NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KOSA KISHERIA. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA
USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU MAPEMA
ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA
NA:
DCP:
AHMED MSANGI.
KAMANDA
WA POLISI (M) MWANZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.