Shughuli ya kutoa heshima na kuuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC Morgan Tsvangirai imefanyika kwenye viunga vya mji mkuu Harare.
Hayati Tsvangirai alifariki dunia Jumatano iliyopita ya tarehe 14 mwezi huu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi thakili ya saratani.
Kiongozi huyo wa upinzani, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 65 ametajwa kuwa ni 'Jenerali wa Watu' aliyewaongoza katika harakati raia masikini wa Zimbabwe, wafanyakazi wa vibarua na vijana tokea mwaka 1988.
Wakati wa uhai wake, hayati Morgan Tsvangirai pamoja na wafuasi wake walipigwa, walidhalilishwa na hata kutuhumiwa kwa mashtaka ya uhaini katika enzi za utawala wa Robert Mugabe.
Bi Chioniso Mazivanhanga, mama wa miaka 59 ambaye anasema alikuwa akimjua Morgan Tsvangirai tangu mwaka 1976 alipokuwa kiongozi wa jumuiya wa wachimba migodi, amemuomboleza mwanasiasa huyo kwa kusema: "Tsvangirai hakumbagua yeyote. Alimpenda kila mtu".
Rais Emmerson Mnangagwa, siku ya Jumapili alifika nyumbani kwa hayati Tsvangirai kutoa mkono wa pole na kuiahidi familia yake kuwa serikali italipia gharama zake zote za matibabu.Hayati Morgan Tsvangirai, enzi za uhai wake. |
Maziko ya Morgan Tsvangirai yanafanyika leo kijijini kwao Buhera mahali alikozaliwa, yapata kilomita 200 kusini mashariki mwa mji mkuu wa Zimbabwe.
KWA HISANI YA http://parstoday.com/sw/news/africa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.