ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 27, 2018

KIRINGO ANYIMWA DHAMANA NA KURUDISHWA TENA RUMANDE MPAKA TAREHE 13-03-2018.

kiringo
Mahakama  ya  mkoa  mjini  magharibi vuga  imekataa  dhamana  ya  Hassan  Aboud  Talib  (Kiringo ) na   kurudishwa  tena  rumande  mpaka  tarehe  13  03  2018  kwa  ajili  ya  kupisha upepelezi wa  mlalamikaji kutokamilika. Kuskiliza  mashtaka  yake.

Hakimu  wa    mahkama  ya  mkoa  vuga  aliendesha  kesi  hiyo    Valentina  Andrew  kasema   ametoa  ufafanuzi  maelezo  ya  upande  wa  mshtakiwa  na  mlalamikaji ambapo  wakili  wa  mshatakiwa  rajab  abadalalh  ambaye  aliiambia  mahakama  hiyo kuwa  mteja  wake  ana  haki  ya  kupatiwa  dhamana  na kutokana  na  kuto kamilika  ushahidi kwa walalamikaji.

Akiendelezea mamuzi ya makahakam hiyo hakimu valesine amesema wakili wa upande wa serikali  Hassan  Ali  Mohd  ameambia  mahakama  hiyo  kwamba  mshatakiwa  huyo  akipewa  dhamana   kutokana  na  kosa  la  kumlawiti  mtoto   ambapo kwa sasa matendo hayo yamekithiriki katika jamii, hivyo endapo akipewa dhamana   jamii itaweza kujichukulia hatua mikokoni kwa kumdhuru   hivyo  mahakama  hiyo ikatae  dhamana  mpaka  utakapo  kamilika  ushahidi.

Hakimu wa mahakama hiyo Valestine amesema baada ya kuridhia pande zote mbili dhidi ya mshatikwa huyo mamuzi ya mahakama kuzuia dhamana hiyo ili kupisha shughuli za upelelezi zitakapokamilika.

Baadhi  ya  wananchi  wamefurahishwa  na  maamuzi  yaliyotolewa  na  mahkama  kuu   na  kumuomba  rais  wa  zanzibar  na  mwenyekiti  wa  baraza  la mapinduzi    Zanzibar  Dr  Ali  Mohammed  Shein  kutia  saini  sheria   iliyopitiswa  na   wajumbe  wa  baraza  la wakilishi  zanzibar.

Kati ya kesi zilizowasilishwa mahakam hapo  jana kesi kumi na tatu zimehairishwa huku nyengine zikiendelea kusikilizwa mahakamani hapo kwa mahakimu mbalimbali.


Vitendo  vya  udhalilishaji  vimeenegeza  kwa  kasi  kubwa  katika  jamii  hivyo  ni vyema  kwa  serikali   ya  mapinduzi  ya  zanzibar   kuweka  adhabu  kali  kwa  watuhumiwa  wanaofanya  vitendo  hivyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.