ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 22, 2018

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa  zana haramu za uvuvi  kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita .

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu.

Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo.

Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi  kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu .

Na,Joel Maduka,Geita.
Serikali Mkoani Geita Imeteketeza  zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila  zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.

Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi  huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika  kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel  Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa  hifadhi ya Rubondo  wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi  na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la  "KIFUNDA"

Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na  taratibu za sheria  askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.


Aidha Mageni aliongeza kuwa  katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na  baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa mapato.

Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha  watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.

Nyawalwa Wange  ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema  agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.

Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni  zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.