Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akionyesha fimbo ya kimasai baada ya kupewa cheo cha kiongozi wa kimila Olaigwanani rika ya Korianga akizungumza na wakazi wa akiwa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Na Mathias Canal, Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu
utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na
uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya
watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na
wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani
Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la
Longido.
Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa
ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu
yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa
maslahi ya Taifa.
Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi
kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa
ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt
Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka
2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.
Alisema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria
dhidi ya yeyote atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya
uchaguzi.
"Ndugu zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na
kuwahakikishia kuwa MTU yeyote atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya
uchaguzi anapaswa kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa
Kheri
Alisema kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa
kusimamia vyema asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na
Halmashauri sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu
na imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.
Aliongeza kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na
Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi
ya Jimbo atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi
muhimu na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.
Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu
likiwemo Jimbo la Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13
Januari 2018.
Wakati huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor
Mwenyekiti Kheri amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika
kusimamia vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo
kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.