TAREHE 29.01.2018
NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
MHE.Shanif Mansoor Mbunge wa Jimbo la Kwimba, leo amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Mtemi Msafiri wakati akiwa katika ziara zake jimboni humo na kufanya kikao kukutana na kamati ya ulinzi na usalama.
Mwenyekiti wa kikao hicho cha ndani ambaye ni mkuu wa wilaya husika Mhe. Mtemi Msafiri ataja moja ya malengo ya kuketi kwao katika meza moja ni kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo la Kwimba na kuzitolea maazimio, pamoja na kuhakiki utekelezaji wa maazimio yaliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri akisalimiana na mzee wa Jimbo.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akisalimiana na mmoja wa wazee wilayani humo.
Makaribisho yakifanyika ndani ya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri kabla ykutia saini kitabu cha wageni. .
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akitia saini katika kitabu cha wageni ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri akiongoza kikao cha Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya yake akiwemo mbunge wa Jimbo hilo Shanif Mansoor aliyeketi kuia kwa Mkuu wa wilaya.
Shanif Mansoor Mbunge katika picha ya pamoja na kamati.
Shanif Mansoor Mbunge katika picha ya pamoja na kamati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.