ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 29, 2018

ETHIOPIA KUWAACHIA HURU MAELFU YA WAFUNGWA WA UPINZANI.

Ethiopia kuwaachia huru maelfu ya wafungwa wa upinzaniSerikali ya Ethiopia imetangaza kuwa itawaachia huru wafungwa waliotiwa nguvuni kufuatia machafuko ya mwaka 2015 na 2016 yaliyotokea katika eneo la Oromia.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Addisu Arega Kitessa amesema kuwa wafungwa 2,345 wamesamehewa na wataachiwa huru siku chache zijazo.
Habari hiyo ya kusamehewa maelfu ya wafungwa nchini Ethiopia imetangazwa wiki moja baada ya kuachiwa huru kinara wa upinzani wa watu wa kabila la Oromo, Merera Gudina na wenzake 22 ambao makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema walikuwa wafungwa wa kisiasa. 

Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa karibu wafungwa elfu mbili wa kisiasa wangali wanashikiliwa katika jela za Ethiopia.  
Kabla ya hapo Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn alikuwa ametangaza kuwa serikali yake itawaachia huru wafungwa wa kisiasa ili kujenga maridhiano ya kitaifa na kupanua demokrasia nchini humo.





Hailemariam Desalegn

Gudina alikamatwa mwaka 2016, baada ya kukosoa rekodi mbaya ya haki za binadamu ya serikali ya Addis Ababa na hali ya kisiasa nchini Ethiopia.
Askari usalama wa serikali ya Ethiopia wamekamata makumi ya maelfu ya watu na kuua waandamanaji zaidi ya 900 tangu yalipoanza maandamano ya watu wa Oromo waliokuwa wakipinga unyakuzi wa ardhi zao, ukandamizaji wa kisiasa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.