ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 7, 2018

AZAM FC YAICHAPA SIMBA KIMOJA NA KWENDA NUSU FAINALI MAPINDUZI



TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji chipukizi Iddi Kipwagile aliyefunga dakika ya 59 akimalizia pasi ya kiungo Frank Domayo ‘Chumvi’.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa ikikamilisha mechi zake nne za Kundi A kwa ushindi wa mechi tatu na kufungwa moja na URA ya Uganda.

Simba inabaki na pointi zake nne baada ya mechi tatu, ikishinda moja na sare moja na itaingia kwenye mchezo wake wa mwisho na URA Jumatatu kusaka lazima ushindi ili kwenda Nusu Fainali.

Kocha Mrundi wa Simba SC, Masudi Juma alitoa walinzi wengi na kuingiza washambuliaji wengi kipindi cha pili kulazimisha bao la kusawazisha, lakini Azam FC walikuwa makini kuzuia mashambulizi yote.

Na sifa zaidizimuendee kipa Mghana, Razack Abalora aliyeokoa michomo mingi ya hatari hata akashinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi baada ya mchezo huo.

Mchezo uliotangulia wa Kundi B, Singida United iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya JKU mabao ya Daniel Lyanga dakika ya 19 na Elinywesia Sumbi dakika ya 20.

Singida United wanafikisha pointi 12 baada ya mechi zao nne na watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na Yanga SC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tisa Jumatatu. Singida na Yanga zimekwishafuzu Nusu Fainali.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Salmin Hoza, Yahya Zayed/Frank Domayo dk55, Bernard Arthur na Iddi Kipagwile/Bryson Raphael dk81.

Simba SC; Emanuel Mseja, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Moses Kitandu dk68, Juuko Murshid, Asante Kwasi/Erasto Nyoni dk64, Jonas Mkude, James Kotei/Mwinyi Kazimoto dk72, Muzamil Yassin, John Bocco, Said Ndemla/Laudit Mavugo dk61 na Shiza Kichuya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.