NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya
VIWANGO
vya madhara ya kuumia vinahusika sana katika kufikia matokeo ya tathmini
anayofanyiwa mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi, Daktari bingwa mbobezi wa
mifupa na viungo nchini, Dkt. Robert Mhina, (pichani juu), amesema.
Dkt.
Mhina ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada juu ya misingi inayopaswa
kuzingatiwa na daktari au mtoa huduma ya afya wakati akimfanyia tathmini
mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi, kwenye mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa
na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uwezo madaktari na
watoa huduma za afya kutoka mikoa ya nyanda za juu Kusini yanayoendelea kwenye
ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya.
Akifafanua
Dkt. Mhina alisema, Viwango vya fidia vitatofautiana kulingana na viwango vya
madhara aliyopata mtu kulingana na kazi anayofanya. “Mfano dereva aliyevunjika
mguu ambao anautumia kukanyaga klachi na gia katika kazi yake, fidia yake
haiwezi kulingana na mhudumu wa ofisi ambaye naye amevunjika mguu” Alisema na
kufafanua kuwa.
“Dereva
hawezi tena kuendelea na kazi yake ya udereva kwa vile hana mguu tena ambao aliutegemea
kufanya kazi, lakini mhudumu anaweza kutumia gongo na akatembea, ingawa muda wa
kufika mahala fulani katika ofisi utakuwa tofauti, lakini anaweza kuhamisha
mafaili kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kwa maana hiyo bado ataendelea
kufanya kazi hiyo tofauti na dereva.” Alisema
Kwa
msingi huo, Dkt. Mhina ambaye pia ni mshauri wa masuala ya tiba alisema “Wananchi
na wafanyakazi wanapaswa kujua kuwa mafao yatatolewa kutegemea na athari au
kazi mtu anayofanya na hayawezi kufanana katika kupiga hesabu za kutoa mafao,
kwani kuna vitu vya ziada vinapaswa kuzingatiwa pia.
Akifafanua
zaidi kuhusi misingi hiyo ya ulipaji fidia, Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini
wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema, zipo njia kadhaa zinazotumika kulipa
fidia na kutaja baadhi yake kuwa ni fidia anayolipwa mfanyakazi aliyepata
ulemavu baada ya kuumia,(impairment base approach) ambayo ndiyo inayotumika
sasa kwa mujibu wa sheria katika kulipa fidia, na nyingine ni ile kupoteza kipato kutokana na
ulemavu wa kuumia mahala pa kazi, (wage loss approach)
“Unaweza
ukapata ulemavu lakini bado kipato chako kiko pale pale, na kwa sheria za sasa ingawa
bado kipato chako ni kile kile licha ya kuumia, na kwakuwa sheria ya fidia
inatambua njia ile ya (Imparement base approach), basi mfanyakazi huyo atalipwa
fidia”. Alisema Dkt. Omar.
Hata
hivyo Dkt. Omar alisema, zipo nchi nyingine ambazo zinatumia mfumo huo wa pili
wa mfanyakazi aliyeumia lakini kuumia huko hakupunguzi kipato chake, (wage
loss), hawatoi fidia.
Dkt. Mhina (kulia), na Dkt. Hussein, wakimsikiliza Dkt. Kishashu, wote hawa ni wawezeshaji wa semina hiyo.
Dkt. Hussein Mwanga, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya maradhi ya ngozi na kansa mahala pa kazi.
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Mshiriki akizungumza
Mshiriki akizungumza
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia madai ya fidia (Claims), Bw.Lembo, akizungumza
Baadhi ya washiriki.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusoianio WCF, Bi. Laura Kunenge, akizungumza.
Dkt. Mhina akitoa "somo" kwa washiriki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.