ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 18, 2017

MAHAMAMA KUU YA TANZANIA YAMUACHIA HURU SHEIKH PONDA.

Habari kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es salaam leo ambapo imeamuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamuhuri kupinga Hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyomuachia huru Ponda.

Sheikh Ponda ameachiwa huru mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.

“Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi nakubaliana na uamuzi huo, hivyo namuachia huru,” – Jaji Mkasimongwa

Miongoni mwa hoja alizozitoa Jaji Mkasimongwa ni kwamba upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.

Katika mashtaka yaliyokuwa yakimkabiri katika Mahakama ya Morogoro, Sheikh Ponda anadaiwa August 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Pia inadaiwa aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.

Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa May 9, 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.

Kosa jingine inadaiwa  August 10, 2013 katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.