Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza kuwa, jumla ya watu 18 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya
Afya ya nchi hiyo imetangaza kuwa, kuanzia tarehe Mosi Septemba hadi
tarehe 31 Oktoba mwaka huu ambayo ni miezi iliyoshuhudia mvua nyingi
nchini humo, jumla ya kesi 570 ziliripotiwa kuhusiana na ugonjwa huo
ambapo 18 ni kati ya walipoteza maisha.
Kadhalika wizara hiyo imewataka
viongozi pamoja na wananchi hususan katika maeneo ya vijijini kuchukua
tahadhari za kiafya kwa lengo la kuzuia kuenea zaidi maradhi hayo.
Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa wakiendelea kupata matibabu. |
Ugonjwa wa kipindupindu umekuwa
ukizisababishia hasara kubwa ya kiroho na kifedha katika nchi nyingi
masikini hususan za bara la Afrika. Kwa mujibu wa Shirika la Afya
Duniani WHO, licha ya kuboreka hali ya afya duniani, hadi sasa zaidi ya
watu milioni mbili hawapati maji safi ya kunywa suala linalochangia
kukumbwa na ugonjwa huo. Dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni mwathirika
kutapika, kuharisha na kupoteza nguvu nyingi mwilini.
KWA HISANI YA:- Parstoday Swahili
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.