Mbali na kufanya upekuzi, Jeshi hilo linaishikilia simu ya mkononi ya Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa upelelezi huku yeye akisema mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yamezingatia uhuru uliopo katika Katiba.
Upekuzi huo ulifanyika jana mchana muda mfupi baada ya Zitto kwenda kuripoti Kitengo cha Uhalifu wa Makosa ya Kifedha-Kamata jijini humo na kutakiwa kurejea tena Novemba 21.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema ‘’polisi walifika hapa saa 6 na wamefanya upekuzi na wamechukua flash, laptop (kompyuta mpakato) na nyaraka ambazo ni taarifa kwa umma iliyotolewa kuwa tutakutana kujadili hali ya uchumi.”
Ado amesema upekuzi huo ulitumia muda mrefu baada ya polisi hao aliodai walikuwa wanne kufika na Katibu Mkuu wa chama hicho, Doroth Semu kutomkuta hivyo wakaamua kumfuata nyumbani kwake Tabata.
“Walisema watakwenda kufanyia kazi vifaa hivyo na watavirejesha haraka ila hawajasema hasa ni lini...wale polisi mmoja alivaa sare na watatu walivaa kiraia ,” ameongeza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.