NA. ZEPHANIA MANDIA WA
G.SENGOBLOG.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela jana alikutana na jopo la wakaguzi kutoka makampuni mbalimbali yanayofanya biashara na Kiwanda cha kusindika Nyama cha jijini Mwanza cha CHOBO INVESTIMENTS LTD ambapo mkuu huyo ametumia fursa hiyo kujadili mipango na wakaguzi hao katika kuzitangaza fursa za uwekezaji wa viwanda zilizopo mkoani kwake.
Hatua hiyo ya Mongella imekuja kama sehemu ya harakati za mkoa kufikia malengo yaliyowekwa na Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuagiza kila mkuu wa mkoa nchini kujenga viwanda vipya 100 katika kipindi cha mwaka mmoja kinachoanzia Desemba 2017.
Ndani ya Ofisi za Mhe. Mongela kikao kimefanyika.
Wakaguzi kutoka makampuni mbalimbali ya wafanyabishara toka nchi za Falme za Kiarabu, na Australia ambao walikuwa wameambatana na mwekezaji mzalendo John Chobo wa Kiwanda cha kusindika nyama kilichopo Kigongo wilayani Misungwi mkoani hapa cha CHOBO INVESTMENTS wamemweleza mkuu huyo kuwa ujio huo umekuja kama sehemu ya kushuhudia ubora wa kiwanda hicho ambacho kwa sasa kimekuwa tegemeo kwa kiasi fulani katika kulisha soko la nchi zao.
“Miundombinu ya Kiwanda inaweza kuchinja zaidi ya ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko kubwa sana kwa wakulima wadogo na wakubwa wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hali itakayounga mkono juhudi za Serikali ya Viwanda na TADB katika kuboresha minyororo ya thamani kwenye sekta ya mifugo,” alisema Chobo.
Wageni wengine walioambatana na mmiliki wa kiwanda ni pamoja na Ali Ahmed Warsama Auditor kutoka Austeria, Tahir Saleh Hashim kutoka Dubai.
"Tumeona mengi ya kuvutia, tumejifunza mengi,nakwenda kutoa ripoti nyumbani, na nina hakika wawekezaji watakuja Mwanza kuwekeza" Mmoja wa wajumbe hao kutoka nchi za Falme za Kiarabu alisema mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, wakati wa ziara yao kuangalia ubora wa nyama inayozalishwa na kiwanda cha Chobo Investiments .
Licha ya Usafi na Ubora unaoendana na viwango vya kimataifa katika uhifadhi wa vyakula, John Mongela ameonyesha kuridhishwa kwake na mwendelezo wa ubora katika uwekezaji wa Kiwanda cha Nyama
cha Chobo kilichombo Misungwi jijini Mwanza na pia kwa upande wa pili kikiwahakikishia
wakulima wadogo na wakubwa masoko ya mifugo yao.
Mngela amefunguka zaidi na kusema kuwa Kiwanda
cha Chobo ambacho kinamilikiwa na kijana mzalendo, John Chobo kina uwezo
mkubwa wa kusadia wakulima wadogo kwa kununua mifugo yako hivyo
kuwapatia fursa za masoko wakulima hao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.