Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akizungumza Machache wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika katika nyanja ya urembo.
Mwanzilishi wa Chuo cha Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akiwa na Wageni Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy
Baadhi ya Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam
Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akitoa Cheti kwa Mmoja wa Wahitimu Kwenye Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty Academy..
Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja
Chuo cha Manjano Beauty Academy kimetunuku Astashahada (Certificates) na Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.
Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Manjano Beauty Academy iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri, tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,” alisema Shekha.Kwa mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi bora wanaopatikana katika sekta ya urembo ambayo yatawatasaidia wao kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
“Naamini kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili kutimiza ndoto zao.
“Katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio na ajira,” alisema Shekha.
Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.
Aliongeza kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.