Airtel yatoa rai kwa shule Kinondoni kujifunza TEHAMA
Shule
za msingi za Manispaa ya Kinondoni zimeshauriwa kutumia fursa ya
maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo
kwenye manispaa hiyo ili kuweza kujifunza na kupata ujuzi wa Tehama kwa
waalimu na wanafunzi pia.
Wito
huo umetolewa na Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde wakati
akiongea na waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kijitonyama
Kisiwani baada ya kuitembelea na kutambulisha maabara hiyo. Maabara hiyo
ni ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na Atamizi ya Teknohama ya Dar
es Salaam (DTBi) kuhakiksha kuwa Jamii inakuwa na uelewa wa Tehema kwa
mafanikio yao na taifa kwa ujumla.
Tunayo
Idadi kubwa ya waalimu na wanafunzi ambao Tayari washaanza kupata
mafunzo hayo lakini wengi wao wametokea kwenye shule ya Kijitonyama
ambapo hii maabara ipi. Naomba kutoa wito wangu na nyinyi mtumia hii
fursa na mpate mafunzo ya Tahema na ikizingatiwa shule hizi ni majirani.
Ni
furaha kwa wanafunzi hawa kupata mafunzo ya Tehama kwa umri mdogo kwani
inawaraihishia maisha yao ya masomo ya baadae. Pia, kuna wanafunzi
wengine wanakuwa na uelewa mkubwa kwenye mafunzo ya matendo kuliko
nadharia, hii ndio sehemu pekee kwa wanafunzi wa shule ya msingi kupata
mafunzo hayo, aliongeza Matinde.
Matinde
aliongeza kuwa bado mafunzo yataendelea hata baada kuwa shule
zimefungwa kwa ajili ya likizo ya krismas na mwaka mpya na hivyo wito
kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba ,
wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha
jamii hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya
technologia na Tehama kwa ujumla.
Kwa
upande wake, Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Kijitonyama Kisiwani
Sikudhani Semka alitoa shukrani kwa kampuni ya Airtel kuweza
kuwatembelea na kuitambulisha maabara hiyo shuleni kwake. ‘Nachukua
fursa hii kuwashukuru wenzetu wa Airtel. Hapa shuleni kwetu tunao
kompyuta tano lakini hakuna hata moja ambayo inatumika sababu ikiwa
hakuna mwalimu mwenye ujuzi wa kuitumia. Tutamia fursa na kujifunza
mambo ya Tehema ili na sisi tuende na wakati, alisema Semka.
Kwa
upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema
“Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa yeyote ambaye atayejiunga nasi.
Tuhahakisha kuwa kila anayekuwa anapata mafunzo ya hali ya juu na
kuelewa kabisa ili nao waweze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi
wenzao
Jengela
alisema mafunzo yanayotolewa ni pamoja na lego Robotics, program za
uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D
objects” msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program
mbali mbali
Bado tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www.airtelfursa.com au kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.