Na Charles Mseti
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imewataka
wafanyabiashara wakubwa na wa kati kuzingatia bei elekezi ya uuzaji wa
mbolea na uhifadhi wa mbolea kama taratibu za uhifadhi zinavyoelekeza
ili wakulima waweze kupata mavuno mengi na kukuza pato la Taifa.
Agousti 18, mwaka huu, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
Dk. Charles Tizeba alitangaza bei elekezi ya uuzaji wa mbolea nchini,
baada ya kodi mbalimbali za uingizaji wa mbolea kuondolewa ili
upatikanaji wake uweze kuwa rahisi zaidi.
Pia imesema mfanyabiashara yeyote yule atakaebainika kuuza
mbolea kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, atachukuliwa hatua ikiweni kufikishwa
mahakamani mara moja.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkaguzi wa Mbolea wa mamlaka
hiyo, Raymond Konga, wakati wa Oparesheni ya kuwabaini wafanyabiashara
ambao hawafuati bei elekezi ya uuzaji wa mbolea kwa wakulima,
ilioendeshwa jijini hapa.
Konga amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kukagua
kuangalia kama wafanyabiashara wa mbolewa wanafuata bei hiyo elekezi
katika kuelekea katika msimu wa kilimo mwishoni mwezi huu.
"Sisi hapa leo tunakagua kama bei elekezi ya mbolea ya
kupandia na kukuzia mazoa inafuatwa na kama mlivyojionea wenyewe, baadhi
ya wafanyabiashara ikiwemo kampuni ya Matuyuni Agrochemical wao
tumebaini wanahifadhi vibaya mbolea yao.
"Baada ya hali hiyo tumeamua kuchukua hatua ya kufunga
ghala la kuhifadhia mbolea, kwa sababu mmiliki huyu (Matuyani Laizer)
anahifadhi chini ya sakafu kinyume na taratibu zinavyoelekeza uhifadhi
wa mbolea lazima iwekwe juu ya mbao," amesema Konga.
Konga amesema ukaguzi huo ambao umeanzia mkoa wa Shinyanga
na kuendeshwa katika wilaya zake zote, huku akidai kwamba zoezi hilo ni
endelevu kwa mikoa ya kanda ya ziwa na nchini kwa ujumla.
Hata hivyo, amesema lengo la kuendesha oparesheni hiyo kwa
wafanyabiashara hao ni kuhakikisha wakulima nchini wanaweza kununua
mbolea bora kwa bei elekezi ambayo ni nafuu ili wakulima waweze kupata
mavuno mengi.
Mmoja wa wauzaji wa mbolea jijini hapa, Matuyani Laizer,
alisema bei hiyo elekezi, itasababisha nchini kwenda kufa kutokana na
wafanyabiashara walio wengi watashindwa kuuza mbolea kwa kuwa hakuna
faida wanayoipata kwa uuzaji mbolea huku akiiomba serikali kuangalia
upya bei hiyo.
Bei elekezi iliyotolewa na Serikali kwa uuzaji wa mbolea
aina ya DAP kwa jiji la Mwanza ni Sh. 55, 438 na mbolea aina ya UREA ni
Sh. 42, 859 huku wilaya nyingine za mkoa huo zilizobaki bei ikiwa ni
tofauti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.