Skauti wa mkoa wa Mara wakiingia katika himaya ya Nyumba ya Baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kufanya matembezi ya amani ya kilomita 22 kutoka Kiabakari hadi Mwitongo wilayani Butiama mkoani humo, kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 18 iliyopita katika Hospitali ya St. Thomas Nchini Uingereza.
Ni msafara - Skauti wa mkoa wa Mara wakiingia katika himaya ya Nyumba ya Baba wa
Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kufanya matembezi ya
amani kutoka Kiabakari hadi Mwitongo wilayani Butiama mkoani humo.
Rashid Gewa ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa CCM ndiye aliyepokea matembezi hayo ya Kumuenzi Hayati Baba wa Taifa mara baada ya Vijana wa Skauti mkoani Mara baada ya kufanya matembezi ya amani ya kilomita 22 kutoka Kiabakari
hadi Mwitongo wilayani Butiama mkoani humo, kumuenzi Hayati Baba wa
Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 18 iliyopita
akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya St. Thomas Nchini Uingereza na baadaye kuzikwa wilayani humo .
BOFYA HAPA KUSIKILIZA ALICHOSEMA
Skauti kwa umakini na ukakamavu wakimsikiliza Mjumbe huyo.
Mwanahabari kutoka Jembe Fm Albert G. Sengo mbele ya nyumba yenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jana kwenye maadhimisho hayo 14 Oct 2017 Butiama mkoani Mara.
Wanafunzi kutoka Ukerewe mkoani Mwanza nao walisafiri hadi Butiama kudhuru kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa na kisha kushiriki ibada maalum iliyofanyika kwenye kanisa lililo hatua chache toka kwenye himaya hiyo.
Maelezo kwa ufupi pamoja na historia vilianikwa.
Umakini katika kusikiliza.
Albert G. Sengo mbele ya kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mjini Butiama.
Marabaada ya kujumuika pamoja kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Skauti hao walielekea Kanisani kushiriki Ibada maalum.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.