BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na salama ambaye ni pia na Mbunge wa Jimbo ya Ilemela Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akisoma maelezo ya jiwe la Msingi alilozindua.
Kaguhwa Nyamhogolo Octoba 4, 2017 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imekabidhi mradi wa maji safi wenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa wakazi wa Kaghwa Nyamhogolo Wilayani Ilemela, Mkoani Mwanza.
Msaada huo ni sehemu ya jitihada za SBL kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwenye sehemu zenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu. Ukiwa na uwezo wa kuhudumia watu 7,560, mradi huo unahusisha kisima, pampu ya maji pamoja na tanki lenye uwezo kuzalisha maji lita 4,000 kwa saa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi, Hawa Nadan ambaye ni Meneja miradi na uwajibikaji katika jamii SBL aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL John Wanyancha alisema, mradi huo unaojulikana kama ‘Maji ni Uhai’ ni mmoja kati ya miradi ambayo SBL inaifadhili kwenye mikoa kama Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvunma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watu milioni moja.
Aliongeza, mradi wa Kaghwa Nyamhogolo hautasaidia tu kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo, bali pia utaongeza uzalishaji mali kwa kuwa wasichana na akina mama hawatatembea tena umbali mrefu kutafuta maji na kuongeza kuwa utawapa wasichana muda zaidi wa kuhudhuria shule.
SBL inayo sera inayolenga kuboresha maisha ya jamii zetu na Maji ni Uhai ni moja kati ya vipau mbele ambavyo vimeelezewa kwenye malengo ya kampuni yetu kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguka,” alisemaWanyancha
Aidha alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na Kutoa ujuzi kwa ajili ya Maisha, Utunzaji wa Mazingira na Unywaji wa Kiasi.
Zaidi, Nadan alisema SBL inao mpango wa kusaidia wakulima ambao kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita umefanikiwa kuwafikia na kuwasaidia wakulima 100 kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha hivyo kuweza kuboresha maisha yao na ya jamii zao
“Kupitia mpango huu, SBL imeweza kupata malighafi kwa ajili ya uzalishaji wake kutoka tani 0 hadi 10,000 zinazozalishwa na wakulima wa ndani jambo ambalo limesaidia ukuwaji wa kampuni na kuongeza kipato kwa wakulima pia,” alisema.
“Ukiachana na kuchangia uchumi wa nchi kupitia ulipaji kodi, SBL inatoa mchango wake kwa maendeleo ya nchi haswa kwa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama hapa nchini,” aliongeza
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni pia na Mbunge wa eneo hilo Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula aliishukuru SBL kwa msaada huo muhimu na uliokuwa unahitajika sana na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kimaendele inayoigusa jamii
Safi makofi tafadhali. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.