ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 4, 2017

VINARA WA KAMBI YA UPINZANI GABON WAZUIWA KUTOKA NJE YA NCHI.

Vinara wa kambi ya upinzani Gabon wazuiwa kutoka nje ya nchi
Idadi kadhaa ya wapinzani wa serikali ya Gabon wamepigwa marufuku kutoka nje ya nchi kwa tuhuma za kufanya uchochezi, kuvuruga usalama na kuanzisha uasi wa kijamii. 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Gabon, Jean-Eric Nézingi amesema kuwa, kinara wa kambi ya upinzani Jean Ping na maafisa wengine kadhaa wa kambi hiyo wamepigwa marufuku kutoka nje ya nchi kutokana na kuhamasisha uasi na machafuko tarehe 18 Agosti mwaka huu.

Jean Ping ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuanzia mwaka 2008 hadi 2012 amekataa kutambua rasmi matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi mpinzani wake, Ali Omar Bongo na amekuwa akiwahimiza wananchi kufanya uasi wa kijamii. Ping anasema Ali Bongo alifanya udanganyifu katika uchaguzi huo wa mwaka jana.

Jean Ping na Ali Bong.
Taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Katiba ya Gabon imesema kuwa, Ali Bongo alishinda uchaguzi huo kwa kupata asimilia 50 ya kura huku mpinzani wake, Jean Ping akipata asilimia 47.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.