ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 10, 2017

RC TABORA AAGIZA WAKULIMA WA PAMBA WAANDALIWE MAPEMA ILI KUPATA MAVUNO MAZURI.

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeawaagiza Maafisa Ugani kuanza mapema maandalizi ya kilimo cha pamba kwa wakulima kutoka wilaya tano mkoani hapo zilichaguliwa kulima zao ili waweze kuzalisha pamba nyingi na nzuri kwa ajili viwanda mbalimbali hapa nchini.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga wilayani Igunga ambacho kimekuwa hakifanyi kazi kwa miaka zaidi ya 20 kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa pamba ya kutosha.

Alisema kuwa watendaji wote wanaohusika na usimamizi wa zao la pamba ni vema wakahakikisha kuwa wakulima wanapanda mbegu zinazotakiwa na kwa nafasi inayoshauri kitaalamu na kutimia mbolea na dawa za kuua wadudu zinazotakiwa.


Sehemu ya shehena ya mbegu za pamba zinazoota bila kuwa na shaka aina ya UKM 08.
Mwanri alisema kuwa Tabora imepata mbegu bora tani 500 ambazo zitasaidia kusambazwa katika Wilaya ambazo zimechaguliwa kulima zao la Pamba za Kaliua, Urambo, Nzega, Igunga na Uyui.
Alisisitiza pamba itakayolimwa na kuvuna itauzwa kupitia Vyama vya Ushirika na sio vinginevyo ili kuepuka mkulima kunyonywa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alipiga marufuku matumizi ya mbegu ambazo hazikuidhinishwa na Bodi ya Pamba na kuingiza mkoani hapa dawa ambazo zimepitwa na wakati.

 
Mtaalamu wa mawasiliano toka moja ya mashirika nchini Uingereza yaliyojikita kusaidia ukuzaji na urejeshaji wa heshima ya zao la pamba nchini Tanzania kupitia Bodi ya Pamba Bw. Kyaruzi, akiwa ameshikilia zo hilo kwenye moya ya ginneries zilizoko Kanda ya Ziwa.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.