Mkuu wa mkoa
wa Mwanza JOHN MONGELA amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 20 kwenye mitaa ya Ibanda
na Swila kata ya Nyegezi jijini Mwanza hii ikiwa ni kusababisha wananchi wa mitaa hiyo
kukosa huduma muhimu za kijamii na kiuchumi ikiwemo shule,soko pamoja na
zahanati.
Mgogoro huo
ulisababishwa na baadhi ya wananchi kujenga nyumba za makazi kwenye maeneo ya umma yaliyotengwa kwa ajli ya
huduma za kijamii ambapo MONGELA ameamuru huduma hizo zijengwe kwenye maeneo ambayo hayajaendelezwa.
Mitaa ya
ibanda na swila kata ya nyegezi jijini mwanza haina huduma za kijamii na
kiuchumi baada ya maeneo yaliyokuwa yametengwa tangu mwaka 1999
kwa ajili ya ujenzi wa shule,zahanati,barabara,soko pamoja na kituo cha
polisi kujengwa nyumba za makazi.
Uvamizi wa
maeneo hayo umemlazimu mkuu wa mkoa wa mwanza JOHN MONGELA kufika kwenye mtaa
wa ibada kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Kufuatia
kuendelezwa kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii na
kiuchumi, MONGELA ameamuru kubadilishwa kwa matumizi ya baadhi ya maeneo ambayo
hayajaendelezwa.
Hapa MONGELA akatoa fursa kwa wananchi ambao walifunguka vyema nacho kilio cha
malipo ya fidia nacho kikaibuka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.