Meneja Bidhaa wa Kwanza Advertising Network, Leon John akieleza namna ya jukwaa hilo litakavyofanya kazi ambapo mtandao huo utaunganisha kampuni za uzalishaji, wachapishaji mtandaoni na wate |
Baadhi ya wachapishaji (Blogers) wakifuailia kwa makini uzinduzi huo katika hafla iliyofanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt |
Mkurugenzi mtendaji wa KONCEPT na katibu wa Tanzania Blogers Network Bw. Krantz Mwantepele (wa kwanza kulia) akichangia jambo kuhusu uelewa wake juu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa upande wa Blog.Meneja bidhaa kutoka Kwanza Advertising Network, Leon John (wa kati kati)
Meneja Mawasiliano wa Kwanza Advertising Network, Herman Mkamba akieleza vigezo vitakavyotumika kuchagua mitandao na Blog zitakazo jiunga kwenye jukwaa hili.
Meneja Bidhaa wa Kwanza Advertising Network, Leon John akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Kwanza Advertising Network. |
Dar Es Salaam Septemba 18, 2017: Kampuni ya matangazo ya Kwanza Advertising Network, leo imezindua huduma mpya, itakayowezesha biashara mbali mbali na watangazaji kuwafikia mamilioni ya wateja kupitia simu za mkononi, tovuti na mtandao wa intaneti
Akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Hotel jijini Dar Es Salaam, Afisa mtendaji mkuu wa Kwanza Advertising Network Edwin Bruno alisema, huduma hiyo itakuwa na uwazi wa hali ya juu kwa kuwa itamwezesha mtangazaji kuona namna ambavyo tangazo la biashara yake linavyosoma na hivyo kujua ni watu wangapi wameliona na kulisoma
“Kwanza imewezesha blogers wa Tanzania wakati pia ikitumia tovuti zenye kutembelewa na watu wengi kuongeza thamani kwa watangazaji kulingana na wateja wao,” alisema Bruno na kuongeza kuwa Kwanza ni mtandao wa kipekee unao mhakikishia mtangazaji faida kwa kila tangazo analoliweka kwenye mtandao huo.
Bruno alifafanua kuwa, lengo la Kwanza ni kuhakikisha kuwa wateja wake (watangazaji) wanatumia kikamilifu fursa zilizopo katika ulimwengu wa kidijitali kutangaza biashara zao kupitia njia za kisasa za utangazaji ambazo ni pamoja na matumizi ya mtandao.
Zaidi alifafanua kuwa, Kwanza inatumia nyenzo za kisasa ambazo humpa taarifa mteja juu ya watu walioliona au kulisoma tangazo lake na pia kumwonyesha tovuti ambazo tangazo lake limesomwa kwa wingi zaidi.
Alieleza kuwa, Kwanza imegundua namna ambavyo inaweza kuwasaidia watangazaji na wachapishaji kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao.
Kwanza inatoa nafasi kufikia wateja wengi kwa watangazaji na pia kipato kikubwa kwa wachapishaji .Watangazaji kila mara hutafuta namna ya kuwafikia wateja wao kwa kiwango kikubwa na hii ni nafasi kubwa kwa wachapishaji wa Tanzania kutumia fursa hii kwa makini kutengeneza kipato zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.