ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 10, 2017

KABURI LA HALAIKI LA MAITI 110 LAGUNDULIWA KATIKATI MWA BURUNDI.


Kaburi la halaiki la maiti 110 lagunduliwa katikati mwa BurundiMkuu wa Kamisheni ya kubaini ukweli na Maridhiano ya Kitaifa nchini Burundi, ameelezea habari ya kugunduliwa kaburi la halaiki lililozikwa ndani yake watu 110 katikati mwa nchi hiyo.

Jean Louis Nahimana, Mkuu wa Kamisheni ya kubaini ukweli na Maridhiano ya Kitaifa yenye makao yake mjini Bujumbura, mji mkuu wa Burundi amesema kuwa idadi ya makaburi ya umati yaliyogunduliwa katika mkoa wa Mwaro, katikati mwa Burundi yanaonyesha kuwa akthari ya mauaji hayo ya halaiki yalitokea kati ya miaka 1972 na 1993.

Ramani ya Burundi.
Nahimana amesisitiza kuwa, raia wa Burundi wamebainisha mahala yalipo makaburi hayo lakini hakuna maelezo zaidi yatakayotolewa hadi utakapofahamika ukweli halisi kuhusu makaburi hayo ya halaiki. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika, karibu watu 4792 wakazi wa mikoa ya Mwaro na Karuzi walipoteza watu wa familia zao katika mauaji ya mwaka 1962. 

Kamisheni ya kubaini ukweli na Maridhiano ya Kitaifa nchini Burundi, ina jukumu la kufanya uchunguzi kuhusiana na jinai na wahusika wa mauaji ya umati yaliyojiri kuanzia tarehe mosi Juni 1962 wakati nchi hiyo ilipopata uhuru hadi tarehe 4 Desemba 2008.
 Raia wa Burundi katika machafuko.
Burundi imekuwa ikikumbwa na migogoro tofauti yakiwemo mauaji ya umati katika vita vya kikaumu kati ya Wahutu na Watutsi yaliyopelekea malaki ya watu kuuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi nje ya nchi hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.