Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi, Sambaru na Mulumbi kwa ajili ya kulipa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd.
Wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi,
Sambaru na Mulumbi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza
katika
mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd.
Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mining Ltd Philbert
Rweyemamu akielezea utaratibu wa ulipaji fidia kwa wanufaika.
Wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi,
Sambaru na Mulumbi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza
katika
mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd.
Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mining Ltd Philbert
Rweyemamu mara baada ya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa uchimbaji madini.
Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wananchi mara baada ya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa uchimbaji madini.
Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi, Sambaru na Mulumbi kwa ajili ya kulipa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd.
Wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi,
Sambaru na Mulumbi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza
katika
mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd.
Na Mathias Canal,
Singida
Kampuni ya
Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold Mining Limited) iliyopo katika
kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida huenda
ikaanza uchimbaji wa madini ya dhahabu hivi karibuni baada ya kuanza kulipa
fidia ya zaidi ya Bilioni 1.6 wanufaika wa awamu ya pili inayohusisha wananchi
kutoka Vijiji vitatu vya Mang'onyi, Sambaru na Mulumbi.
Kampuni hiyo
tayari imekamilisha ulipaji wa awamu ya kwanza kwa kulipa zaidi ya Milioni
900.2 Wanufaika waliolipwa fedha hizo wanaotokana na mazoezi mawili ya uthamini
yaliyofanywa kwenye eneo la mradi kwa ajili ya upanuzi wa kambi.
Malipo hayo
yatakamilisha umiliki wa maeneo hayo kwa Kampuni ya Shanta Gold mining kwa
ajili ya uchimbaji na kuwafanya wananchi hao kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu
pasina kinyongo chochote.
Malipo hayo ya
awamu ya pili na ile ya kwanza yamelipwa kwa wanufaika wote wa fidia katika
Vijiji vyote vilivyopo Katika Kata ya Mang'onyi yanaondoa malalamiko ya muda
mrefu ya wananchi wa maeneo mbalimbali waliopo kwenye eneo la mradi huo
waliotaka kufahamu hatima ya malipo yao.
Akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi na
wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa kampuni hiyo
inapaswa kutumia muda mfupi katika ulipaji wa fidia kama ilivyofanya katika
awamu ya kwanza.
Alisema kuwa
Kampuni hiyo ya uchimbaji imeanza kutekeleza sheria ya madini inayoelekeza
miezi sita kabla ya kuanza uchimbaji wawekezaji wanapaswa kuanza kulipa fidia.
Naye Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mining Ltd Philbert
Rweyemamu alisema kuwa kampuni yake imeanza kutekeleza maelekezo yaliyotolewa
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu mwezi Disemba 2016 ya
kuwalipa wanufaika hao fidia ambayo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi
huo.
Alisema kuwa
malipo yanafanywa na kampuni hiyo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya sambamba na wenyeviti wa
serikali za vijiji vyote vilivyopo ndani ya mradi.
Kuanza kwa
uchimbaji wa madini katika eneo hilo kutaibua ajira nyingi kwa wananchi
Wilayani Ikungi na Taifa kwa ujumla jambo litakalosaidia ukuzaji wa pato la mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.
Katika Awamu ya
Kwanza Kampuni ya Shanta Gold Mining Ltd iliwalipa wanufaika 92 wenye umiliki
wa Viwanja 121 thamani yake ikiwa ni Shilingi 902,412,247.00 Hulu awamu hii ya
Pili wakilipwa Wamiliki 114 wenye Viwanja 156 vyenye thamani ya Shilingi
1,663,112,018.01
Aidha, Kuanzia leo
Septemba, 2017 wanufaika wa fidia wameanza kufanya uhakiki wa malipo yao na
ufunguaji Akaunti kwa ajili ya malipo ikiwa ni matakwa ya kisheria.
Akizungumza kwa
niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mang'onyi Ndg Mohamed H. Ramadhani
alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kutoa
maagizo ya kulipwa haraka fidia za kila wanufaika Jambo ambalo limetekelezeka
kwa haraka katika kipindi Cha muda mfupi.
Sambamba na hayo
aliongeza kuwa Mkuu huyo wa Wilaya anafanya kazi kubwa katika kuwaunganisha
wananchi wote ili kupata stahiki zao na kufurahia Rasilimali za Nchi yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.