ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 24, 2017

DPP WA KENYA AAGIZA UCHUNGUZI DHIDI YA MAAFISA WA NAGAZI ZA JUU WA IEBC.

DPP wa Kenya aagiza uchunguzi dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa IEBCMkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma nchini Kenya (DPP), Keriako Tobiko ameagiza polisi na Kamisheni ya Maadili ya Kupambana na Ufisadi EACC kuanzisha uchunguzi dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, kutokana na kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Tobiko amewapa Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Ndegwa Muhoro na Halakhe Waqo, Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC siku 21 kukamilisha uchunguzi huo.
Katika barua yake kwa maafisa hao, Tobiko amesema, kwa mujibu wa Ibara ya 157 (4) ya Katiba, na Sheria ya Makosa ya Uchaguzi  ya mwaka 2017, anataka uchunguzi huo ufanyike ili kubaini iwapo makosa ya jinai au makosa mengine yalifayika katika uchaguzi huo wa mwezi uliopita au la.
Haya yanajiri siku chache baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kubadilisha tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio wa urais hadi Oktoba 26 mwaka huu na sio Oktoba 17 kama ilivyotangaza hapo awali.

Majaji wa Mahakama ya Juu Kenya.
Mahakama ya Juu ya Kenya mapema mwezi huu ilitengua ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Agosti 8 ikiashiria kuwepo kasoro na kuiamuru IEBC kuandaa uchaguzi wa marudio ndani ya siku 60. 
Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa Agosti 8, atachuana na hasimu wake kutoka muungano wa Nasa, Raila Odinga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.