Mkazi wa
kitongoji cha Endevesi ,kata ya Oljoro wilaya ya Arumeru, Hwanga Ndaskoy (30) amevunjika
mguu wake wa kulia baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni askari polisi mkoani
Arusha, wapatao nane kumvamia na kumpiga risasi ,akiwa shambani kwake .
Akizungumza kwa
masikitiko nyumbani kwake, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mount Meru
alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja,Ndaskoy ameeleza kwamba tukio hilo limetokea mnamo,Agost
31,mwaka huu majira ya saa saba wakati akivuna mahindi shambani kwake akiwa na familia yake.
Alisema kua alifuatwa na askari hao waliokuwa wamevalia kiraia na mmoja mwenye silaha akiwa amevaa sare za kipolisi.
Alisema kua alifuatwa na askari hao waliokuwa wamevalia kiraia na mmoja mwenye silaha akiwa amevaa sare za kipolisi.
Pia askari hao walikuwa wameongozana na mkazi mmoja wa kitongoji hicho aliyemtaja kwa
jina la ,Yohane Palay aliyemtambua kuwa ni baba mkwe wake .
‘’Nilimsikia
baba mkwe akiwaelekeza askari hao wanikamate huku akiwatahadhalisha kuwa mimi
ni mkorofi na wasinisogelee nitawakata na sime jambo ambalo sio kweli,ndipo
askari mmoja mwenye silaha aliponifyatulia risasi ya mguu na kuanguka chini’’alisema Ndaskoy
Aidha
alisema askari baada kumpiga risasi walimpakia kwenye gari lao na
kumpeleka katika hospital ya Mkoa Mt,Meru ambapo walimweleza daktari
kuwa ameanguka na pikipili Jambo ambalo si kweli.
Alieleza
kuwa kabla ya tukio hilo ,Agost 26 mwaka huu ,aligombana na mke wa kaka yake
aitwaye ,Jehova Baraka ambaye wanaishi jirani baada ya mbuzi kula mahindi
yake yaliyokuwa nyumbani .
Alisema
ugomvi huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kutoleana maneno makali ,ambapo Jehova
aliamua kwenda kwa baba yake mzazi aitwaye Yohane Palay na kutoa taarifa kuwa
amepigwa na shemeji yake .
Palay
aliamua kwenda kituo cha polisi cha Mbauda jijini hapa na kutoa taarifa
juu
ya tukio hilo,hata hivyo viongozi wa kitongoji hicho wakiwemo wazee wa
ukoo waliingilia kati na kumtaka Palay alirejeshe nyumbani ili wazee wa
ukoo walipatie
ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo waliafikiana.
Alisema Kikao
cha ukoo kiliketi,agost 30 na kukubaliana kumaliza jambo hilo kwa kuwatoza
faini za kimila wahusika wote wawili baada ya kubaini wote wanamakosa,hata
hivyo walishangaa kesho yake agost 31 kufuatwa na polisi na kupigwa risasi.
Kwa upande
wake,Palay alikiri kupeleka malalamiko yake kituo cha polisi ,Mbauda ,akidai
kuwa mtoto wake,ambaye ni mke wa kaka yake na majeruhi alipigwa na
kudhalilishwa. Hata hivyo aalikana kuwarubuni Polisi ili wampige risasi mtuhumiwa
Akizungumzia
tukio hilo,kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema kuwa
anafuatilia undani wa tukio hilo ikiwemo kubaini ni askari gani walienda kwenye
tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi.
"Kwa kweli sina taarifa ya tukio kama hilo ila nitachunguza kama lipo nitalitolea ufafanuzi" Kauli ya Mkumbo.
Mkumbo alisema
analifanyia uchunguzi jambo hilo kupitia
wasaidizi wake na kuahidi kuchukua hatua kali iwapo itabainika hapakuwa na
ulazima wa matumizi makubwa ya silaha ya moto kwa askari wake.
Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.