ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 23, 2017

SIMBA KUWAKOSA HAWA WAWILI.

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco anatarajiwa kuikosa mechi ya watani wa Jadi 'Ngao ya Jamii' inayochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kutokana na kutokuwa vizuri kiafya.

Hayo yamebainishwa na Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja wakati alipokuwa anazungumza na mashabiki zao kupitia mtandao wao na kusema wamejiandaa vizuri kuwapa raha mashabiki watakaojitokeza uwanja wa Taifa kutazama mtanange huo kwa kuwa wanakikosi kizuri kilichokamilika.

"Sisi kama Simba tunahitaji ushindi katika mechi ya leo kwa sababu itatusaidia kutuweka katika nafasi nzuri huko mbeleni. Wachezaji wote wako vizuri kasoro wawili ambaye ni John Raphael Bocco pamoja na Said Mohamed. Nawaomba mashabiki wa Simba waje kisimba kisimba kuipa ushirikiano timu yao iwapo uwanjani ili wachezaji waweze kufanya vizuri zaidi ya vile walivyopanga kufanya leo", alisema Mayanja.

Kwa upande wake, Nahodha wa Simba Method Mwanjali amesema wamejipanga vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo imekuwa yenye kutazamwa kwa jicho pana na mashabiki wao ili waweze kupata furaha ya ushindi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.