ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 28, 2017

SIERRA LEONE:- IDADI YA WAHANGA WA MAPOROMOKO YA UDONDO IMEPITILIZA ELFU MOJA.

Serikali ya Sierra Leone imetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyoambata na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown imepindukia elfu moja. 

Maafisa wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maafa hayo imepindukia elfu moja hususan kwa kutilia maanani mamia ya watu waliotoweka na hawajulikani waliko hadi hii leo.

Takwimu zilizotolewa na waziri wa serikali ya Freetown zinaesema kuwa, hadi sasa  zaidi ya watu elfu moja wamethibitika kuwa waliaga dunia kutokana na maporomoko ya udongo ya mji wa Regent.

Awali shirika la Hilali Nyekundu la Sierra Leone limetangaza kuwa watu wasiopungua elfu tatu wamepoteza makazi yao kutokana na maafa hayo ya maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown na kwamba watu wengine 500 hawajulikani waliko.

Maiti za wahanga wa maafa ya Sierra Leone Maporomoko hayo yaliambatana na mvua kali na mafuriko yalitokea wiki mbili zilizopita nchini Sierra Leone.
 
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga wa maafa ya hayo.

 Jeshi la Sierra Leone na timu za uokoaji zinaendelea na kazi ya kutafuta wahanga wa maafa hayo makubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.