ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 4, 2017

RC MAKONDA APOKEA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye tamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Vitanda hivyo ambabyo pia vina Magodoro pamoja na Mashuka yake vitapelekwa kwenye Wodi mpya ya Mama na Mtoto iliyojengwa kwenye Hospital ya Amana chini ya ufadhili wa kampuni ya Amsons Group ambayo ujenzi wake umekamilika kwa Asilimia mia moja.
Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwaajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli” Alisema Makonda.

“Tumedhamiria kuhakikisha Mama,Mtoto na Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es salaam wanapata huduma bora, na huduma bora zipo kwenye Afya,kama Wagonjwa wasipopata huduma bora inakuwa ni tatizo,tayari kama mnavyofahamu tuna Majengo ya kisasa tunayoendelea kujenga Chanika, Amana, Temeke na Mwananyamala ambapo kukamilika kwake yataongeza tija ya upatikanaji wa huduma za bora za Afya, sasa Vitanda hivi 150 ni tafsiri tosha kuwa vinakwenda kupunguza adha kwa kinamama wanaokwenda kujifungua kwenye Hospital ya Amana” Aliongeza Makonda.
Kwa upande wake Suleiman Amour meneja uendelezaji wa biashara kampuni ya Camel Oil amesema vitanda hivyo ni uendelezaji wa kutoa mchango wao kuunga mkono juhudi za mkuu wa mkoa za kuhakikisha wananchi wa Dar es salaam wanapata huduma bora za afya.

Ikumbukwe kuwa Kampuni tanzu ya Mafuta na Saruji za Amsons Group ndio wanaojenga wodi za mama na motto kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala baada ya mkuu wa Mkoa kuwashirikisha dhamira yake ya kumaliza kero kwenye sekta ya Afya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.