ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 24, 2017

RAIA 12 WATIWA MBARONI MISRI KWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA VIUNGO VYA BINADAMU.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kuwa, imewatia mbaroni watu 12 wakiwemo madaktari na wauguzi kadhaa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya magendo ya viungo vya binadamu.

Duru za habari zimeinukuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ikitangaza habari hiyo na kueleza kuwa, miongoni mwa waliotiwa mbaroni ni madaktari watatu, wauguzi wanne, mfanyakazi mmoja wa hospitali na madalali wawili. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ni kuwa, kundi hilo lilikuwa na nia ya kuuza viungo vya binadamu nje ya nchi na kujipatia fedha nyingi.

Baadhi ya watuhumiwa hao walitiwa mbaroni wakati walipokuwa katika operesheni ya kutoa viungo vya mwili vya raia wa Misri kama figo na moyo katika moja ya hospitali binafsi.

Maandamano ya kupinga biashara ya viungo vya binadamu 
 
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO, Misri ni miongoni mwa nchi ambazo biashara ya magendo ya viungo vya binadamu imeenea mno.
 
Mwezi Disemba mwaka jana pia Wizara ya Afya ya Misri ilitangaza habari ya kugunduliwa mtandao mkubwa zaidi ya kimataifa unaofanya bishara haramu ya viungo vya binadamu na kueleza kuwa, watu 45 walitiwa mbaroni kwa kuwa na uhusiano na mtandao huo.

Uuzaji wa viungo vya mwili wa binadamu umekuwa njia inayowawezesha mamilioni ya wananchi wa Misri kujikimu kimaisha. Raia wengi wa Misri wanaishi chini ya mstari wa umaskini kutokana na hali mbaya ya uchumi wa nchi yao. Viungo vya binadamu vinavyouzwa katika bishara hii ni pamoja na moyo, figo, bandama, macho na kadhalika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.