CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan
maeneo ya wilayani na vijijini imekuwa ni moja kati ya masuala yanayo kwamisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi na baadhi ya watendaji wa serikali.
Watumishi wa serikali mathalani Maafisa Mifugo, Madaktari na Maafisa Elimu wamekuwa wakishindwa kufanya ukaguzi wa maeneo yao ya kazi, kusimamia ama kufanya ufuatiliaji wa utendaji kutokana na changamoto ya usafiri, lakilini kupitia mpango huo mwanga wa matumaini umeanza kuonekana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete amekuja na mpango mkakati wa kusaidia watendaji wa ndani wa Halmashauri ya Jimbo lake kwa kuwawezesha vitendea kazi kurahisisha usafiri na utoaji huduma kwa kuwapatia pikipiki ili wafanye kazi vyema kwa wakati.
"Tulianza kuwapa pikipiki maafisa Mifugo wetu wanne na baada ya kukusanya nguvu ya kutosha tumewapatia pikipiki watendaji hawa 10 ili kukamilisha idadi ya watumishi 14 katika halmashauri"
"Kwanini tumechagua usafiri huu wa pikipiki? Sote tunafahamu unafuu na urahisi wa kuuhudumia usafiri huu hadi service. Tofauti na magari kwa mafuta kiasi kidogo unaweza kutumia pikipiki kufanya mizunguko mingi yenye manufaa na tija kwa watu wetu" alisema Mbunge huyo.
Kwa mujibu wa Ridhiwan amesema kuwa awamu inayokuja ni kuwaangalia Watendaji wa Kata zote ili kuweza kuwafikia wananchi waliomchagua.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.